Mambo makubwa hayatakiwi papara!! Sababu zilizofanya MAANDAMANO yabume

0 2 Comments

Hamjambo wapendwa?? Leo nimeona ngoja nichukue mda kidogo kuchambua sababu haswa zilizo sababishia MAANDAMANO maalum yaliyotakiwa kufanyika siku ya UHURU day kubuma. Kwanza kabisa, nianze kwa kusema nampa HONGERA dada wa Taifa (Kama vile wafuasi wake wanavyomwita) kwani kitendo alichojaribu kufanya na kuhitimisha ni kizuri na kimempa ushujaa, ijapokuwa mambo hayakwenda kama yeye na wafuasi wake walivyotegemea.

Watu wanaweza kusema, ooh kutokana na vitisho vilivyotolewa na Serikali pamoja na mkuu wa polisi juu ya maandamano ndo kisa kilichofanya maandamo kutoenda vizuri. Ila, cha muhimu na chakuangalia ninini kilikosekana kwenye uharakati huu toka mwanzo. Kwani ilikuwa ni UONGOZI BORA, MAANDALIZI na BUSARA.

Namaanisha nini kwa kusema UONGOZI BORA? Well, kama kiongozi wa group la wanaharakati wa aina yoyote, unatakiwa kuwa na delegates ambao come high, come low, watakuwa bega na wewe. Lakini, toka mwanzo, dada wa Taifa hakuliweka hilo jambo sawa. Na alipokosea zaidi tena, ni pale alipoanza kutukana watu matusi. Hapo ndo alipo chapia kabisaa. Kwani, hakuna mtu mwenye akili yake timamu hata awe na hasira vipi na nchi au uzalendo wake uwe mkubwa kiasi gani, atakubali kuwa bega na mtu ambaye anaendesha vitu kiholela. Watu wanaheshima zao, wanaakili zao na wana wajibu zao.

Hakuna mtu mzima na timamu katika fahamu anayependa kujiletea matatizo. Kwani, watu wanataka kutatua matatizo na sio kuwa chanzo cha matatizo. Kwamaana ukumbuke watu kama wakina Mbowe, Zitto, Ms. Mdee, Tundulisu na wengine wengi tuu wamekuwa wanaharakati katika Siasa toka miaka na miaka, sio wajinga na sio wapumbavu, kwamba hawayajui matusi. Ila, wanaelewa maana ya Demokrasia na Diplomasi. Sasa, kama “dada wa Taifa” angekuwa na upeo wa maana kichwani toka mwanzo alipoamua kuwa mwanaharakati, hawa ndo watu ambao juzi alitakiwa awe amewavuta na wangekuwa bega kwa bega nae katika kile kinachoitwa UZALENDO. Kwamaana si uongo, dada wa Taifa ana jua ku-move watu. Lakini tatizo lake ni kwenye circle yake hana watu wamaana waku msaidia kumuvisha hoja. Hana watu reliable ambao wamejikita kwenye siasa na wakati huo huo ni pia wanaharakati.

MAANDALIZI – Maandamo si kitu cha mchezo. Lazima mtu ujiandae. Alichotakiwa kufanya dada wa Taifa,  ili kupata support nzuri na kubwa kila kona mfano wa Marekani. Alitakiwa a-deligate watu ambao pamoja nao, wangesaidiana kutafuta viongozi wote wa vikundi/vyama vya watanzania chini Marekani. Angehakikisha kila jimbo Marekani limekuwa contacted. Tena yeye kama ingewezekana ange-fanya ile phone call ya kwanza halafu awaache aliowadelegate wafuatilie na kuweka mambo mengine sawa. Angeomba ushirikiano wa viongozi wa hivi vyama/vikundi na angeomba wa-wahamasishe wanachama wao wote watoe  maoni yao na ushirikiano wao kadri iwezekanavyo ili kuweza kufanikisha jambo hili muhimu siku iliyokuwa imeandaliwa. Na kwa wale ambao wangeweza kwenda DC basi wafanye hima.

Alitakiwa ku-make sure simu zinapigwa kila siku kufuatilia watu na kuhakikisha wako teyari kushiriki na kukamilisha hili tukio. Lakini nadhani yeye alifikiria just through IG watu watakurupuka. Ukumbuke, mfano hapa Marekani, mtu kuomba tuu sick leave kazini unajiuliza mara mia mia. Hapo ni unaumwa, unaweza kupoteza kazi hivi hivi unajiona. So, kama haku-allow watu kujiandaa, nobody will just quit a day off work ili kwenda kwenye maandamano ambayo yanaweza yakakumtokea puani baadae. Kitu kingine dada yetu anaishi hapa Marekani, labda yeye ana mamilioni na bili zake zimeshakuwa taken care of, watu wengi hapa kazi ni kuchakarika ili waweze kumudu maisha na wengi wanafamilia. Sasa wewe unapokuja na hoja zako ambazo si mbaya lakini hujajipanga inakuwa ni issue kupata wafuasi.

Pia, kama mfano kwa huko Tanzania, alitakiwa awe na watu (viongozi) wa maandamano. Hii inasaidia kuwa na spokes person (muongeaji) mkuu iwapo mtu anatakiwa kuongea na vyombo vya Habari. Pia kama vile VOA walivyojaribu kumuhoji dada wakati yupo pale DC akiandamana, dada alitakiwa atoe neno moja ama mawili tuu halafu aseme, atapenda kukaa chini na vyombo vyovyote vya habari ili aonglee kwa undani juu ya MAANDAMANO na HOJA zilizofanya kuita maandamano hayo. Kama wewe ndo mkuu wa maandamo hiyo ndo njia moja kuu ya kupata exposure na hoja yako kupewa masikio ya watu.

Ni obvious kwamba dada hakufanya utafiti (research) yake vizuri hapa hapa alipo na kuomba ushirikano kutoka kwa wanaharakati wa mataifa menine ambao wanaelewa vizuri mambo ya maandamano. Kwani angesaidiwa sana tuu kutokana na sababu ya maandamano ni ya msingi. Hapo napo alichapia. It takes a village!!!

Hivyo basi, nataka nieleweke kwamba NI ASILIMIA KUBWA YA WATANZANIA MAREKANI NA KWINGINE KOTE WANAO UDHISWHA NA MAMBO AMBAYO YAMEKUWA YAKIENDELEA HUKO TANZANIA. Na wanasupport HOJA YA KUTAKA RAISI AJIUZULU. Na just because hawakujitokeza siku ya maandamano haimaanishi kwamba HOJA HAIKUWA NA WAKEREKETWA wengi.

BUSARA – busara haitokani na mtu kwenda shule. Busara eidha una zaliwa nayo ama unajifunza kuwa na busara. Kuna watu wengine wanashangaza sana, unakuta anasema, eeh, kweli huyu dada chuma, ama huyu dada mdogo lakini katingisha Taifa, ama eh huyu dada kwa kuongea kweli ni mwanaharakati. Na hivyo eti ndo vigezo vikuu kwa watu. Yaani tusishangae kwanini watanzania bado wanaongozwa na CCM na wataendelea kuongozwa na CCM mpaka Yesu atakapo rudi kwa mara ya pili. Kwamaana CCM haijamwacha dada nyuma hata kidogo. Kwani, ndo hivyo hivyo wanavyofanya, maneno mengi ya malumbano wakati wa kampeni, maneno mengi bungeni, wanagawa kanga na pilau wakati wa kampeni ili wapate kura, blah blah blah si ndio? okay, sasa utofauti ukowapi kati ya vigezo vya CCM na watu wanavyotoa juu ya dada wa Taifa? Kitu ni kile kile, malumbano na maneno mengi tu ambayo mara nyingi ni ya kipuuzi kwamaana yamejaa matusi ndani yake.

Hivyo basi, kwa mara nyingine napenda kumpa Dole gumba dada wa Taifa. Kwani alijitahidi na alichojaribu kufanya ni kikubwa. Si watu wengi wanaweza kuwa na msimamo ama nguvu hiyo. Pia ningependa kumfariji aendelee kukazana na uwanaharakati na ajaribu kujiweka vizuri na watu wenye heshima zao/viongozi ndani na nnje ya nchi kwani teyari ana jeshi lake mwenyewe zuri tuu. Anachohitaji tu! ni vichwa vya maana vya kuongoza jeshi lake na hawezi akafanya mambo makubwa peke yake. It takes a TEAM, a very good and organized TEAM!!

Haya basi hayo ndo niliyoyaona mimi sijui wewe. Toa neno lako hapo chini. Nimesema ukweli ama?

 

Categories:

2 thoughts on “Mambo makubwa hayatakiwi papara!! Sababu zilizofanya MAANDAMANO yabume”

  1. B says:

    Interesting..just getting around reading your posts kwenye blog yako

    1. admin2 says:

      Welcome! Thank you for stopping by and for the comment 🙂 There is more to come, keep tuning in. Just briefly, traditionallyMe vision is to eventually tell people’s stories aka life journey’s as our belief is we can all inspire each other through our powerful life stories. Please take time and read our welcome letter in the Home page, Welcome note! We are welcoming suggestions and collaboration(s). Karibu sana na tafadhali share na wengine kuhusu traditionallyMe. Asante sana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *